Waziri mkuu wa Ethiopia akutana na Waziri wa mambo ya nje wa China Addis Ababa
2023-01-11 08:47:20| CRI

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Qin Gang mjini Addis Ababa.

Kwenye mazungumzo yao Bw. Ahmed amesema Ethiopia inatarajia kuimarisha mabadilishano ya uzoefu wa utawala na China ili kuwashikamanisha na kuwaongoza waethiopia wote kushikilia uhuru wao na kuharakisha maendeleo na ustawi wa nchi yao.

Amesema Bw. Qin kuichagua Ethiopia kuwa kituo cha kwanza kwenye ziara yake ya kwanza nje ya nchi baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje, kumeonesha urafiki wa kina kati ya nchi hizo mbili na umuhimu wa uhusiano wao.

Bw. Qin amesema katika zaidi ya nusu karne iliyopita tangu China na Ethiopia zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi hizo mbili siku zote zimekuwa zikisaidiana na kupiga hatua bega kwa bega bila kujali ni vipi hali ya kimataifa inabadilika, na kuweka mfano wa kuigwa wa mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea.