Mjumbe wa China atoa wito wa uungaji mkono wa kimataifa kwa Afrika Magharibi na eneo la Sahel
2023-01-11 08:48:08| CRI

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing ametoa wito wa kufanywa juhudi zaidi kutoa uungaji mkono na misaada kwa amani na maendeleo endelevu katika Afrika Magharibi na eneo la Sahel.

Balozi Dai amesema Afrika Magharibi na eneo la Sahel limepata mafanikio muhimu kwenye kudumisha usalama wa pamoja, kurejesha maendeleo ya uchumi na jamii na kuimarisha mshikamano na ushirikiano wakati wa kukabiliana na hali ya kikanda na kimataifa yenye utatanishi.

Ameliambia Baraza la Usalama kuwa jumuiya ya kimataifa na Baraza la Usalama wanapaswa kuwa na uelewa wa kina zaidi kuhusu changamoto ngumu na mahitaji halisi ya nchi zilizoko kwenye kanda hiyo, kufanya juhudi kubwa kutatua vyanzo vya matatizo, na kutoa uungaji mkono na misaada kwa ajili ya kutimiza amani ya kikanda na maendeleo endelevu.