China yapinga vizuizi vya kibaguzi kwenye forodha
2023-01-11 09:03:17| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema China inapiga vikali baadhi ya nchi zinazotekeleza vitendo vya kibaguzi dhidi ya wachina wanaoingia katika nchi zao na itachukua hatua kujibu vitendo hivyo.

Bw. Wang amesema kwenye mkutano wa kila siku na wanahabari kuwa tangu China itangaze kushughulikia COVID-19 kwa utaratibu wa magonjwa ya kuambukiza ya daraja la B na kupitisha njia za mpito za usafiri wa kuvuka mpaka, nchi nyingi zimekaribisha uamuzi huo lakini baadhi ya nchi zimeweka vizuizi dhidi ya wasafiri kutoka China.

Wakati huohuo ofisa mwandamizi wa Shirika la afya duniani WHO amezitaka nchi mbalimbali kuchukua hatua za usimamizi wa wasafiri kwa mujibu wa sayansi, ambazo ni zenye uwiano na zisizo za kibaguzi.