Waziri wa Mambo ya Nje wa China asema kinachojulikana kama "mtego wa madeni" barani Afrika ni mtego wa simulizi
2023-01-12 11:39:46| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang Jumatano alikanusha madai yasiyo na msingi kwamba China inaunda "mtego wa madeni" barani Afrika, akisema kile kinachojulikana kama "mtego wa madeni" ni mtego wa simulizi uliowekwa dhidi ya China na Afrika.

Qin alisema hayo kwenye mkutano na wanahabari akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat. Amesema katika miaka ya hivi karibuni nchi za Afrika zimekuwa zikijitahidi kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii, lakini ukosefu wa fedha umekuwa kikwazo kikubwa kwa ustawi na ufufuaji wa Afrika, na kusisitiza kuwa namna ya kuweka usawa kati ya fedha za maendeleo na ukuaji wa deni ni suala ambalo nchi zote lazima zikabiliane nalo ana kwa ana katika harakati za kutafuta maendeleo.

Akibainisha kuwa China siku zote inajitolea kusaidia Afrika kupunguza mzigo wake wa madeni, Qin amesema nchi yake ni mshiriki hai katika Mpango wa Kurefusha Muda wa kulipa Madeni wa Kundi la 20 (G20). Pia alisema China imetia saini makubaliano au kufikia makubaliano na nchi 19 za Afrika kuhusu msamaha wa madeni na imesitisha malipo mengi zaidi ya madeni kati ya nchi za G20.