Marais wa China na Angola wapeana salamu za pongezi za kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi
2023-01-12 11:34:24| cri

Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Angola Joao Lourenço leo wamepeana salamu za pongezi za kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili.

Katika salamu hizo rais Xi ameeleza kuwa, anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Angola, na yuko tayari kushirikiana na rais Lourenço kutumia fursa ya kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi, kuimarisha uaminifu wa kisiasa, kukuza ushirikiano wa kunufaishana na kuongeza urafiki kati ya watu, ili kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Angola. 

Kwa upande wake rais Lourenço amesema, Angola inapenda kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na China, kujenga mustakabali wa kunufaishana na kutimiza maendeleo na ustawi wa pamoja, ili kuwanufaisha zaidi watu wa pande zote mbili.