China yatoa mkopo nafuu kwa mradi wa taifa wa mtandao wa broadband Angola
2023-01-12 08:58:42| CRI

China itatoa uungaji mkono wa kifedha kwa mradi wa taifa wa mtandao wa broadband nchini Angola chini ya makubaliano ya mkopo wenye masharti nafuu yaliyosainiwa jana.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Benki ya Exim ya China itatoa mkopo wa dola za kimarekani milioni 249 kwa ajili ya ujenzi wa kebo ya Fiber Optic yenye urefu wa kilomita 2,000 nchini Angola, pamoja na nyingine ya chini ya maji inaounganisha na eneo la Cabinda, na kuboresha mkongo wa mawasiliano wa nchi hiyo.

Makubaliano hayo yalisainiwa na balozi wa China nchini Angola, Gong Tao na waziri wa fedha wa Angola Vera Daves de Sousa mjini Luanda.

Mradi huo utahakikisha ufikiaji wa huduma za mtandao wa kasi kwenye maeneo ya mbali nchini Angola, kupunguza gharama za huduma na kupiga jeki uchumi wa dijitali wa nchi hiyo.