UM watenga fedha kusaidia waathirika wa mafuriko na ghasia Cameroon
2023-01-12 09:22:39| CRI

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa umetenga dola za kimarekani milioni 6 kutoa msaada wa dharura kwa maelfu ya watu walioathiriwa na mafuriko na ghasia nchini Cameroon.

Naibu katibu mkuu Bw. Martin Griffiths ambaye pia ni mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa alitenga fedha hizo kutoka kwa Mfuko Mkuu wa Mwitikio wa Dharura kusaidia watu katika maeneo ya mbali ya kaskazini, kaskazini magharibi na kusini magharibi nchini Cameroon.    Bw. Dujarric amesema fedha hizo zitasaidia kutoa ulinzi, huduma za makazi, msaada wa chakula na lishe.