Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza umuhimu wa kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika
2023-01-12 08:51:57| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amesema China iko tayari kufanya kazi na Afrika kuimarisha ushirikiano kati yao na kuinua kiwango cha ushirikiano katika zama mpya.

Kwenye mkutano wa pamoja na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat, Bw. Qin amesema huu ni mwaka wa 10 tangu mwaka 2013 wakati Rais Xi Jinping alipofanya ziara barani Afrika, na kuweka misingi ya sera ya China kwa Afrika, yaani udhati, matokeo halisi, urafiki na nia njema, kupigania mazuri na kuwa na maslahi ya pamoja.

Amesisitiza kuwa katika kipindi kipya cha historia, China iko tayari kushirikiana na Afrika kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na kuimarisha ushirikiano kupitia Ukanda Mmoja, Njia Moja.