Jeshi la Sudan Kusini latangaza kwisha kutimua wanamgambo walioko katika Upper Nile, Pibor
2023-01-12 09:14:51| CRI

Jeshi la ulinzi la watu wa Sudan Kusini (SSPDF) limesema limewatimua wanamgambo wa kundi la White Army katika jimbo la Upper Nile na eneo la Greater Pibor (GPAA).

Msemaji wa jeshi hilo Bw. Lul Ruai Koang alipozungumza na waandishi wa habari huko Juba amesema kwa sasa utulivu umerejeshwa katika maeneo hayo baada ya wanamgambo wa kundi la White Army kuondolewa. Sasa mashirika ya kibinadamu yanasambaza vifaa vinavyohitajika kwa wakimbizi katika maeneo hayo.

Kundi la White Army lilishambulia kaunti ya Fashoda ya jimbo la Upper Nile mwezi Novemba mwaka jana, na kusababisha raia zaidi ya elfu 30 kukimbia makazi yao, na mwezi wa Desemba lilifanya shambulizi lingine na kusababisha vifo zaidi ya watu 57. Baadhi ya waangalizi wa kisiasa wa Sudan Kusini wameonya kuwa vurugu za kijamii ziliokithiri na kutishia kuharibu makubaliano dhaifu ya amani yaliyosainiwa chini ya shinikizo la kimataifa.