Kenya yatahadharisha dhidi ya msukosuko wa chakula kutokana na kupamba moto kwa ukame
2023-01-12 10:17:48| CRI


Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ardhi kame na nusu kame na maendeleo ya kikanda wa Kenya Bi Rebecca Miano amesema, msukosuko wa chakula katika kaunti kame unaweza kupamba moto wakati msimu wa mvua uliopungua kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, na kusababisha kupungua kwa mavuno ya mazao ya kilimo na kukauka kwa mbuga na vyanzo vya maji.

Bibi Miano amesema makadirio mapya yameonesha kuwa njaa, utapiamlo na ukosefu wa maji huenda vitapamba moto kote nchini Kenya katika msimu huu wa kiangazi.

Amesema kati ya kaunti 23 kame au nusu kame, hali ya ukame ya kaunti 22 imekuwa kali kutokana na upungufu wa mvua katika msimu wa mvua ulioanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana. Ameongeza kuwa kiwango cha kifo cha mifugo katika sehemu kame, kikiongeza njaa, utapiamlo na hasara ya mapato ya wafugaji, huku akionya kuwa kuchelewa kwa mvua  kukiambatana na uvamizi wa viwavijeshi kutazidisha uhaba wa chakula na utapiamlo kwa watoto katika maeneo kame kaskazini mwa nchi hiyo.