WHO yatangaza mlipuko wa Ebola nchini Uganda umekwisha
2023-01-12 12:25:30| cri

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani barani Afrika imetangaza kwamba ugonjwa wa Ebola nchini Uganda umekwisha. Mlipuko wa sasa wa Ebola nchini Uganda ulizuka katika eneo la kati mwezi Septemba mwaka jana. Hadi kufikia mwishoni mwa Disemba mwaka jana, Uganda ilithibitisha watu 142 walioambukizwa Ebola na vifo 56.