Zanzibar yaadhimisha miaka 59 ya mapinduzi kwa mafanikio makubwa
2023-01-13 09:06:10| CRI

Zanzibar imeadhimisha miaka 59 ya mapinduzi ikiwa na mafanikio mengi ya kijamii na kiuchumi.

Akiongea jana usiku Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwepo kwa amani, umoja na mshikamano ni moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka 59 ya mapinduzi. Amesema bila nguzo hizo tatu ingekuwa vigumu kwa Zanzibar kutekeleza mipango ya maendeleo iliyowekwa kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi, na mipango ya maendeleo kuelekea mwaka 2050.

Rais Mwinyi ambaye amewataka wazanzibar kuendelea kuchapa kazi na kuboresha maisha yao, amesema katika mwaka 2021 uchumi wa Zanzibar ulikua kwa asilimia 5.1, ikilinganishwa na asilimia 1.3 ya mwaka 2020, na mwaka huu unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.08.