Pasipoti ya Tanzania ipo kwenye 10 bora barani Afrika
2023-01-13 14:22:48| cri

Pasipoti ya Tanzania imeorodheshwa ya 74 katika orodha ya kimataifa ya usafiri na imedumisha nafasi yake ya tisa kama pasipoti yenye nguvu zaidi barani Afrika.

Ripoti ya Viashiria vya Pasipoti iliyotolewa na Kampuni ya Henley, inaonesha kuwa idadi ya nchi ambazo Watanzania wanaweza kutembelea bila viza, au kupata viza wanapowasili imeongezeka hadi 72. Pasipoti ya Japani ndiyo yenye nguvu zaidi duniani, ikifanya watumiaji wake kufika nchi 193 bila viza, ikifuatiwa na Singapore, Korea Kusini, Ujerumani na Hispania.

Mauritius, ambayo imeorodheshwa ya 34 duniani imeibuka katika nafasi ya kwanza barani Afrika katika viwango vya kila mwaka vinavyotolewa kwa ushirikiano na Chama cha Kimataifa cha Usafiri wa Anga.