Jumla ya mawaridi 3,000 yaliyosafirishwa kutoka Nairobi, Kenya, yamewasili huko Changsha, mkoani Hunan, China, na kuashiria kuwa shehena ya kwanza ya maua kutoka Afrika yanauzwa mkoani Hunan kwa karibu miaka mitatu iliyopita.
Baada ya kupitia taratibu zote za ukaguzi na karantini, maua hayo yatawekwa kwenye soko la maua kabla ya Sikukuu ya Spring ambayo ni sikukuu muhimu zaidi nchini China.
Kutokana na mila za kijadi, Wachina hununua maua kabla ya Sikukuu ya Spring kwa ajili ya mapambo au kuomba bahati nzuri kwa mwaka mpya, na maua mekundu yanapendelewa zaidi.