Wanajeshi 14 wauawa katika mashambulizi mawili ya kigaidi katikati mwa Mali
2023-01-13 09:18:21| CRI

Idara ya habari na uhusiano ya umma ya jeshi la Mali (Dirpa) imesema wanajeshi 14 wa Mali wameuawa katika mashambulizi mawili ya kigaidi.

Taarifa iliyotolewa jumatano usiku na idara hiyo inasema vikosi vya Mali vilichukua hatua kali dhidi ya uvamizi wa kundi la kigaidi lenye Silaha (GAT) Jumanne kati ya miji ya Dia na Diafarab, na pia kati ya miji ya Koumara na Macina.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya wanajeshi 14, wengine 11 kujeruhiwa na gari moja la upande wa jeshi la Mali kuharibiwa, huku magaidi 31 wakiuawa na mmoja kujeruhiwa.