Waziri aipongeza Huawei Tanzania kwa kutoa ujuzi wa TEHAMA
2023-01-13 14:22:00| cri

Naibu Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania, Tao Mian Jumanne alimtembelea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax. Katika mazungumzo yao, waziri alimpongeza kampuni ya Huawei kwa maendeleo ya kiteknolojia na kuitoa kwa Watanzania.

Katika hotuba yake, aliipongeza zaidi kampuni hiyo kwa kuwekeza katika sekta ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia (TEHAMA) nchini humo hasa kupitia miradi yao inayosambaza huduma za kidijitali vijijini.

Waziri aliongeza kuwa Huawei ni kampuni kubwa na wanathamini uwepo wake nchini humo. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ni moja ya vipaumbele vya serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.