Biashara ya nje ya China yaongezeka na kuweka rekodi mpya mwaka 2022
2023-01-13 15:44:13| cri

Takwimu kutoka Idara Kuu ya Forodha ya China (GAC) zimeonesha kuwa, thamani ya biashara ya nje ya China kwa mwaka ilifikia zaidi ya yuan trilioni 40 (sawa na dola za kimarekani trilioni 5.94) kwa mara ya kwanza mwaka 2022, huku nchi hiyo ikiboresha hatua ili kuratibu mapambano dhidi ya COVID-19 na maendeleo ya kiuchumi na kijamii wakati inapokabiliwa na hali ngumu za ndani na kimataifa.

Takwimu hizo zimeonesha kuwa, thamani hiyo ya biashara iliongezeka kwa asilimia 7.7 mwaka 2022 kuliko ile ya mwaka uliotangulia, na kuongoza duniani kwa miaka sita mfululizo.

Msemaji wa Idara Kuu ya Forodha ya China Lv Daliang amesema, biashara ya nje ya China ilipata mafanikio mazuri katika wigo, ubora na ufanisi mwaka jana licha ya changamoto mbalimbali.