Sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Angola yafanyika mjini Luanda
2023-01-13 09:06:48| CRI

Sherehe ya kuadhimisha miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Angola iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Angola imefanyika mjini Luanda ikihudhuriwa na wageni 600 kutoka serikalini, vyama vya siasa, jeshi, mashirika ya China na jumuiya mbalimbali za huko.

Balozi wa China nchini Angola Bw. Gong Tao amesema kwenye hotuba yake kuwa katika miaka 40 iliyopita China na Angola zimekuwa zikifuata moyo wa kushikamana na kunufaishana, na kuweza kunufaika kutokana na ushirikiano na katika maeneo mbalimbali.

Kwa miaka mingi China imekuwa mshirika mkubwa wa biashara kwa Angola, soko kubwa la bidhaa zake, na chanzo kikuu cha uwekezaji. Angola imekuwa mshirika mkubwa wa pili kwa China na muuzaji mkubwa wa pili wa mafuta ghafi kwa China.

Waziri wa mambo ya nje wa Angola Esmeralda da Silva Mendonca amesema urafiki kati ya China na Angola ulioanzishwa Januari 12 mwaka 1963 ni wa kunufaishana, na kueleza imani yake kuwa utaimarisha zaidi urafiki na ushirikiano.