Takwimu kutoka idara ya forodha ya China zinaonesha kuwa, sekta ya biashara ya China imeweza kuhimili changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na kufungwa kutokana na janga la COVID, na mwaka jana thamani ya oda kutoka nje ya nchi ilizidi Yuan trilioni 40 ($ 5.96 trilioni) kwa mara ya kwanza katika historia, ambazo wachumi wanasifu kuwa mnara halisi wa uthabiti wa ugavi wa kimataifa katika miaka mitatu iliyopita.
Wachumi pia wanatabiri kuwa mwaka huu sekta ya biashara ya China itadumisha ukuaji thabiti, hasa baada ya serikali kuboresha usimamizi wa COVID, na kuendelea kuboresha muundo wa biashara wa China..
Takwimu zinaonesha kuwa thamani jumla ya bidhaa zilizoagizwa na mauzo ya nje ya China ziliongezeka kwa asilimia 7.7 mwaka hadi mwaka hadi yuan trilioni 42.07 ($6.26 trilioni) kwa mwaka 2022, na kufikia rekodi mpya. Mauzo ya bidhaa nje ya nchi yalipata ukuaji wa tarakimu mbili wa asilimia 10.5 mwaka jana hadi yuan trilioni 24, huku uagizaji kutoka nje ukipanda kwa asilimia 4.3. Ziada ya biashara iliongezeka hadi yuan trilioni 5.9 kutoka kiwango cha yuan trilioni 5.3 cha 2021, kikionyesha nguvu ya mauzo ya nje ya nchi.