Mgomo wa kupinga hali mbaya ya kiuchumi wadhoofisha sekta muhimu nchini Sudan
2023-01-16 11:47:44| CRI

Mgomo wa kupinga mapato madogo na hali mbaya ya kiuchumi uliofanyika Jumapili umedhoofisha sekta muhimu zaidi nchini Sudan.

Maelfu ya wafanyakazi na wanafunzi mjini Khartoum walilazimika kwenda kazini na shuleni kwa miguu baada ya wamiliki wa mabasi ya usafiri wa umma kuweka mgomo wa kupinga tozo kubwa ya leseni, faini za barabarani na kodi. Zaidi ya asilimia 75 ya watu wanaoishi Khartoum wanategemea mabasi kama njia yao kuu ya usafiri.

Sekta ya usafiri sio pekee iliyoathirika na mgomo, kwani kuna vyuo vikuu vingi vimekuwa vikishuhudia mgomo wa wanafunzi mara kwa mara wakipinga ongezeko la ada. Jumla ya vyama vya elimu 20 vilitoa taarifa Jumapili vikikosoa ongezeko la ada katika vyo vikuu kwa karibu asilimia 800.