Watu wasiopungua 10 wauawa kwenye mlipuko kaskazini mashariki mwa DRC
2023-01-16 11:46:15| CRI

Msemaji wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika jimbo la Kivu Kaskazini Anthony Mwalushayi amesema watu wasiopungua 10 wameuawa na wengine 39 kujeruhiwa vibaya kwenye shambulizi la mlipuko wa bomu lililotokea katika kanisa moja mjini Kasindi, jimboni humo, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa akaunti ya Twitter ya Wizara ya Mawasiliano ya DRC, serikali ya nchi hiyo ililaani vikali shambulizi hilo la bomu la Jumapili lililofanywa na waasi wa kundi la ADF.