China kuboresha uwezo wa huduma za matibabu katika ngazi mbalimbali wakati sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ikikaribia
2023-01-16 11:59:38| CRI

China inaboresha uwezo wa huduma katika ngazi ya jamii na taasisi za matibabu za vijijini ili kukabiliana na changamoto za janga la UVIKO-19 kufuatia sikukuu ya mwaka mpya wa jadi inayokuja hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Afisa wa Kamati ya Afya ya Taifa ya China Jiao Yahui, taasisi hizi za afya zinachukua hatua mbalimbali kuongeza nguvu kazi zao na kuhifadhi dawa. Mamlaka za afya zinasaidia taasisi za matibabu ili ziweze kuwa na vifaa vyao wenyewe. Pia amebainisha kuwa vifaa vya kupimia (oximeters) vimesambazwa katika zahanati za vijiji katika nchi nzima.

Mbali na hapo hospitali za ngazi ya tatu katika maeneo ya mijini pia zimeelekezwa kuanzisha huduma ya saa 24 ya matibabu kwa njia ya simu inayounganishwa na hospitali za kaunti. Mfumo wa kuhamisha matibabu pia umeanzishwa ili wagonjwa wenye dalili kubwa maeneo ya vijijini waweze kuhamishiwa kwenye taasisi za matibabu za mijini kwa wakati.

Pilika za mwaka mpya wa jadi wa China zimeanza Januari 7 mwaka huu baada ya nchi kurekebisha sera yake ya UVIKO-19, ambapo sikukuu itakuwa tarehe 22 mwezi huu.