Somalia yafunga akaunti za benki za kundi la al-Shabaab
2023-01-16 13:02:23| cri

Serikali ya Somalia imesema kuwa imefunga akaunti 250 za benki za kundi la al-Shabaab ili kufunga vyanzo vya fedha vya kundi hilo.

Ofisa wa ngazi ya juu wa Somalia amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kuwa, akaunti 70 za fedha za mtandaoni za kundi hilo pia zimefungwa ikiwa ni juhudi za serikali ya Somalia kuzuia upatikanaji wa fedha.

Somalia imetangaza vita ya wazi dhidi ya wapiganaji wa kundi la al-Shabaab lenye uhusiano na kundi la al-Qaida.