Idadi ya vifo kwenye ajali ya barabarani Nigeria yaongezeka hadi 16
2023-01-16 12:04:15| CRI

Polisi wa usalama barabarani nchini Nigeria wamesema idadi ya vifo kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika jimbo la Plateau, katikati ya nchi hiyo imeongezeka hadi 16.

Msemaji wa Kikosi cha Usalama Barabarani cha serikali ya shirikisho jimboni Plateau Peter Longsan alisema jumla ya watu 99 walihusishwa katika ajali hiyo, kati yao 16 wamethibitishwa kufariki na wengine 83 kujeruhiwa, na kuongeza kuwa ajali hiyo ilisababishwa na kasi kubwa kupita kiasi na ubebaji wa kuzidi uwezo wake.

Longsan aliwaambia waandishi wa habari kwamba lori lilipinduka baada ya dereva kushindwa kulidhibiti katika barabara karibu na kijiji cha Jwak kilichoko katika eneo la serikali ya mtaa wa Mangu siku ya Jumamosi.