Idadi ya waliouawa kwenye shambulizi la Russia dhidi ya mji wa Dnipro nchini Ukraine imeongezeka na kuwa zaidi ya 20
2023-01-16 13:03:43| cri

Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la kombora la Russia katika mji wa kati wa Ukraine wa Dnipro imeongezeka na kuwa zaidi ya 20. Mkuu wa utawala wa kijeshi wa eneo la Dnipropetrovsk, Bw. Valentyn Reznichenko amesema kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Telegram kuwa takriban watu 73 wamejeruhiwa, huku wanne wakiwa katika hali mahututi.

Takriban watu 40 bado hawajulikani walipo kufuatia shambulizi hili lililotokea  jumamosi na kutekeketeza nyumba 72 na kuharibu vingine 230.

Naibu mkuu wa ofisi ya rais wa Ukraine Bw. Kyrylo Tymoshenko, ameandika kwenye Telegram kwamba wafanyakazi wa dharura 530 na watu wanaojitolea na vitengo 144 vya vifaa wanashiriki katika operesheni ya uokoaji. Russia haijatoa maoni yoyote kuhusu shambulizi hilo.