Kampuni ya China kukamilisha kituo kidogo cha kV 400 cha Konza katika mji wa kisasa wa Konza
2023-01-17 10:02:07| CRI

Kampuni ya Ujenzi wa Mambo ya Anga ya China (CACGC) inapanga kumaliza utekelezaji wa kituo kidogo cha kV 400 cha Konza na kuunganisha nyaya za juu katika Mji wa Konza, ambao ni wa kisasa nchini Kenya, hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba.

Meneja wa Mradi wa Upanuzi wa Usambazaji Umeme wa Kenya (KPTEP) Zhu Yunye, amesema ujenzi wa njia ya usambazaji umeme ya Isinya-Konza yenye urefu wa kilomita 40 na kv 400 na vituo vidogo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 70. Mbali na hapo amesema pia wamekusanya karibu asilimia 95 ya vifaa na nyenzo muhimu zinazohitajika kwenye utekelezaji wa mradi huo.

Naye Alex Wachira, Katibu Mkuu wa Idara ya Taifa ya Nishati, amesema kampuni ya China ina uwezo wa kutekeleza mradi ndani ya muda uliopangwa kwa mujibu wa mkataba. Amefafanua kuwa mradi huo ni muhimu kwa Kenya, kwani utatoa umeme wa kutosha na wa kuaminika katika mji huo, ambao ni moja ya miradi mikuu ya nchi hiyo.