Msomi wa Afrika: Jaribio lolote la kuruvuga uhusiano kati ya Afrika na China halitafanikiwa
2023-01-17 14:28:08| CRI

Kuanzia tarehe 9 hadi 16 mwezi Januari, waziri mpya wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang alifanya ziara yake ya kwanza nchini Ethiopia, Gabon, Angola, Benin na Misri na kutembelea makao makuu ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Nchi za Kiarabu. Mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa Mali Prof. Yoro Diallo hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG amesema, ziara hiyo ya Bw. Qin Gang imeenzi desturi ya mawaziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka katika bara la Afrika kwa miaka 33 mfululizo, kitendo ambacho kimedhihirisha kuwa jaribio lolote la kuchafua ushirikiano kati ya China na Afrika halitayumbisha urafiki kati ya pande hizo mbili.

Kwenye sherehe ya kukamilika kwa mradi wa makao makuu ya Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Maradhi cha Afrika (Africa CDC) iliyofanyika Januari 11, Bw. Qin Gang alimesema, China imekabidhi makao makuu ya Afrika CDC kwa marafiki wa Afrika, na yataendeshwa na kusimamiwa kikamilifu na Umoja wa Afrika. Prof. Diallo amepongeza kukamilika kwa mradi huo na kuona kuwa makao makuu ya Africa CDC yatakuwa alama nyingine kubwa ya urafiki kati ya Afrika na China, na mradi huo umeionesha dunia kwa ukweli usiopingika kwamba China siku zote imekuwa ikiiunga mkono Afrika kwa vitendo halisi, na hakuna nguvu yoyote inayoweza kuuzuia uhusiano kati ya Afrika na China kupiga hatua kuelekea siku bora zijazo.

Prof. Diallo amesema, katika miaka ya hivi karibuni ushirikiano kati ya Afrika na China umepata mafanikio makubwa yanayong’ara duniani. Afrika na China zimetekeleza kivitendo “Mipango Kumi ya Ushirikiano”, “Hatua Nane” na “Miradi Tisa”, na kupata matunda mengi kwenye ushirikiano wa kupambana na janga la Uviko-19, na China imekuwa mwenzi mkubwa wa kwanza wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 13 mfululizo. Mwaka 2022 thamani ya biashara kati ya Afrika na China ilizidi dola za kimarekani bilioni 260, na kasi ya ongezeko la uuzaji wa bidhaa za Afrika kwa China imezidi kwa mara nyingine ile ya uagizaji bidhaa kutoka China. Amesema, nchi 52 za Afrika na Tume ya Umoja wa Afrika wamesaini nyaraka za ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na China, huku miradi mikubwa kama vile ujenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kamisheni ya Umoja wa Afrika, reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi na reli ya Addis Ababa-Djibouti ikiendelea kuibuka na kutekelezwa, na miradi ya ushirikiano wa miundombinu ikiwemo barabara, umeme, mawasiliano ya simu na bandari ikisambaa kote barani Afrika, miradi hiyo imeongeza kidhahiri uwezo wa Afrika wa kujitegemea na kutimiza maendeleo endelevu. Prof. Diallo amepongeza mapendekezo manne kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika yaliyotolewa na Bw. Qin Gang kwenye ziara hiyo, na kuona ziara hiyo imeimarisha imani kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya Afrika na China katika siku zijazo.