China kuchukua hatua zaidi kuinua ubora na viwango vya ushirikiano kati yake na Afrika
2023-01-17 13:02:57| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang amefanya ziara ya siku saba kuanzia tarehe 9 hadi 16 katika nchi za Ethiopia, Gabon, Angola, Benin, Misri na kutembelea makao makuu ya Umoja wa Afrika na makao makuu ya Umoja wa Nchi za Kiarabu, kwa lengo la kuimarisha zaidi uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika na kusukuma mbele ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Yuxi amesema, Afrika ni moja ya maeneo ya mwanzo kwenye safari ya diplomasia ya China mpya, na kukuza mshikamano na ushirikiano na nchi za Afrika ni chaguo thabiti la kimkakati na la kudumu la China.

Bw. Liu amesema, katika hali ya kimataifa inayojaa sintofahamu na mabadiliko, China haibadilishi na itaendeleza nia yake ya asili kwenye diplomasia yake. Ameongeza kuwa, safari za kutembeleana kama marafiki na jamaa kama ziara hiyo, ndizo zimejenga urafiki imara usiovunjika kati ya China na Afrika, na kusogeza karibu mioyo ya watu wa China na Afrika.