Serikali ya Uganda yawataka wafadhili kuiunga mkono kupambana na mlipuko wa Ebola katika siku zijazo
2023-01-17 13:04:03| cri

Waziri wa Afya nchini Uganda Ruth Aceng ameataka wafadhili kufikiria kuisaidia Uganda kujiandaa kikamilifu kupambana na milipuko ya Ebola katika siku zijazo.

Akizungumza hivi karibuni, Waziri huyo amesema kuiandaa nchi hiyo kukabiliana na mlipuko mwingine wa Ebola sio tu kwamba unailinda Uganda na athari za ugonjwa huo, bali pia ni kulinda jamii yote ya kimataifa.

Amesema ingawa Uganda imetangaza kumalizika kwa mlipuko wa Ebola, serikali na wenzi wake wanapaswa kuendelea na usimamizi, utafiti wa tiba, chanjo na utambuzi wa ugonjwa huo.