Tanzania kufanya majaribio ya SGR kati ya Dar es Salaam na Morogoro mwezi ujao
2023-01-17 13:05:26| cri

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kuanza majaribio ya kutoa huduma katika Reli ya Kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro mwezi ujao.

Akizungumza na wanahabari mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amesema, kazi ya ujenzi wa SGR, awamu ya kwanza ya reli kilomita 1,219 kati ya Dar es Salaam na Mwanza, na kipande cha kilometa 300 kati ya Dar es Salaam na Morogoro imefikia asilimia 99.77. Msigwa amesema ujenzi wa kipande cha Morogoro hadi Makutupora ambacho ni kilomita 422 umefikia asilimia 91.79, na kipande cha Makutupora hadi Tabora kazi imefikia asilimia 3.95.