Marekani na Japan zahimizwa kuacha kuidhibiti na kuikandamiza China
2023-01-17 10:04:03| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Jumatatu alizitaka Marekani na Japan kuacha vitendo vyao vya kuidhibti na kuikandamiza China, kuacha kulijenga jeshi kwa njia za hatari na kueneza machafuko duniani.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa ya pamoja iliyotolewa hivi karibuni na viongozi wa Marekani na Japan wakidai kwamba eneo la Indo-Pacific linakabiliwa na changamoto zinazoendelea kukua, zikiwemo vitendo visivyoendana na utaratibu wa kimataifa wenye msingi wa kanuni vinavyofanywa na China. Pia wamesisitiza nia yao ya kuimarisha muungano kati ya Marekani na Japan.

Wang amesema vitendo vichafu vya kuipaka matope China vinavyofanywa na Marekani na Japan, kuingilia mambo ya ndani ya China na kukandamiza maendeleo ya China vimejaa hatari na unafiki. Hivyo amesema China inapinga vikali na kwamba itachukua hatua zinazostahiki.