Xi ataka watu wasio wanachama wa CPC kutumikia maslahi ya nchi
2023-01-17 10:00:53| CRI

Rais wa China na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Xi Jinping, amewataka watu wasio wanachama wa CPC kutekeleza majukumu yao kwa juhudi na azma kubwa na kufanya kazi ya kuunganisha nguvu na kutumikia maslahi ya jumla ya nchi.

Xi, amesema hayo wakati aliposhiriki kwenye hafla inayofanyika kila mwaka na watu wasio wanachama wa CPC kabla ya sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Kwa niaba ya kamati kuu ya CPC, Xi ametoa pongezi kwa viongozi wapya waliochaguliwa wa kamati kuu za vyama vingine mbalimbali vya kisiasa na Shirikisho la Viwanda na Biashara la China (ACFIC), na kutuma salamu kwa watu wa vyama vingine vya kisiasa na ACFIC, watu wasio na vyama, na watu walio mstari wa mbele.

Amebainisha kuwa mwaka 2023 ni mwaka wa kwanza wa kujifunza na kutekeleza miongozo ya kanuni za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, kwa matumaini na changamoto kwa pamoja na kutaka kufanywa juhudi za pamoja ili kuboresha hali ya usasa ya China.