Mtandao wa Tik Tok watoa tuzo kwa wabunifu kutoka Afrika
2023-01-17 13:03:31| cri

Jukwaa la video fupi la Tik Tok linalomilikwa na Kampuni ya ByteDance ya China limetoa tuzo kwa wabunifu wa Afrika eneo la Sahara kwa ujuzi wa ngazi ya juu na ubunifu walioleta kwenye jukwaa hilo katika mwaka uliopita.

Hafla hiyo ilifanyika jijini Nairobi, Kenya, kufuatia ushindani mkali wa siku nane wa kura zilizopigwa na watu kupitia jukwaa hilo katika maeneo ya kusini, magharibi na mashariki mwa Afrika.

Mkuu wa Programu ya Ubunifu ya Tik Tok katika kanda Sahara barani Afrika, Boniswa Sidwaba amesema, tuzo hizo ni njia ya Tik Tok kutambua wasimulizi wa hadithi, ubunifu, na athari chanya inayoletwa na wabunifu katika jamii ya Tik Tok.