Mjumbe wa China asema mazungumzo ni njia pekee halisi ya kumaliza mgogoro wa Ukraine
2023-01-18 13:40:41| cri

Naibu mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema, mazungumzo ndio njia pekee halisi katika kutatua mgogoro wa Ukraine.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine, Balozi Dai bing amesema, tangu kutokea kwa mgogoro wa Ukraine, changamoto nyingi zimejitokeza katika pande zote, na mivutano na mapigano kati ya imani tofauti, utamaduni na jamii vimeongezeka.

Balozi Dai amesema China inatumaini kuwa pande zote husika zitajizuia, kuanza mazungumzo, na kuahidi kutatua masuala ya usalama kwa njia za kisiasa. Ameongeza kuwa jamii ya kimataifa inapaswa kujikita katika kuboresha mazungumzo ya amani, kuzishawishi Russia na Ukraine kurejea kwenye majadiliano, na kuweka mazingira ya kusimamisha vita mapema.