Waziri wa Tanzania ataka ushirikiano katika kulinda eneo la Hifadhi
2023-01-18 13:41:57| cri

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka watumiaji wa eneo lililotolewa kwa ajili ya shughuli za ufugaji na kilimo waendelee kulilinda eneo lililobaki kwa ajili ya Hifadhi ya Bonde la Mto Usangu.

Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, alipozungumza na wadau, wawekezaji wa Bonde la Usangu, wakulima wa mpunga, wamiliki wa mashine za kukoboa mpunga na wafugaji Mkoani Mbeya. Dkt Pindi Chana amesema, shughuli za kilimo na ufugaji zisifanyike katika eneo lililobaki ambalo ni chanzo kikubwa cha maji na sehemu ya utalii.