Uganda yaimarisha usalama mpakani baada ya mlipuko nchini DR Congo
2023-01-18 13:41:17| cri

Polisi na wanajeshi wa Uganda wameimarisha ulinzi katika mpaka wa pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea Jumapili.

Msemaji wa jeshi la Polisi la Uganda Bw. Fred Enanga amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Kampala, kuwa hatua zimechukuliwa ili kuzuia uvamizi na mashambulizi katika mpaka wa pamoja wa Mpondwe na maeneo mengine yote. Takriban watu 12 wameuawa na wengine 50 wamejeruhiwa katika shambulizi la mlipuko uliotokea jumapili katika kanisa moja huko Kasindi katika jimbo la Kivu Kaskazini, kaskazini mashariki mwa DRC.