Jeshi la Somalia lachukua mji mwingine ulioshikiliwa na al-Shabab
2023-01-18 10:20:36| CRI

Jeshi la Taifa la Somalia (SNA) linaloungwa mkono na vikosi vya ndani Jumanne limeudhibiti mji wa El-Dhere, uliopo katika jimbo la Galmudug, katikati ya Somalia.

Akithibitisha hayo, Waziri wa Ulinzi Abdukadir Mohamed Nur amesema mji huo ambao ulikuwa mikononi mwa al-Shabab kwa zaidi ya muongo mmoja umerejeshwa baada ya kundi hilo lenye msimamo mkali kuondoka. Bw. Nur ameeleza kuwa kurejeshwa tena kwa mji huo kumekuja siku moja baada ya vikosi vya pamoja kuidhibiti miji ya Harardhere na Galcad.

Kundi la al-Shabab linakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia mashambulizi makali yanayofanywa na vikosi vya serikali ili kuwafukuza katikati ya Somalia.