Naibu Waziri Mkuu wa China Liu He athibitisha tena nia ya China ya ukuaji na ushirikiano wa kimataifa
2023-01-18 10:15:39| CRI

Naibu Waziri Mkuu wa China Bw. Liu He amesema China itaendelea kuchukulia maendeleo ya kiuchumi kama kazi kuu na ya msingi, na maendeleo yenye ubora wa juu ya kiuchumi lazima yawe lengo la China.

Bw. Liu alisema hayo jana alipokuwa akihutubia kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Kiuchumi Duniani huko Davos. Amethibitisha tena nia ya China ya kufungua mlango kwa pande zote, ushirikiano wa kimataifa na nchi nyingine kwa ajili ya utulivu wa kichumi na maendeleo duniani na utandawazi mpya wa kiuchumi. Pia amebainisha kuwa uchumi wa China utashuhudia maendeleo makubwa mwaka huu, na ukuaji wake unaweza kurudi katika hali yake ya kawaida.

Amesema katika miaka 10 iliyopita, pato la taifa la China lilikua kutoka yuan trilioni 54 hadi trilioni 121, wastani wa kuishi wa watu umepanda kutoka miaka 74.8 hadi 78.2, na mchango wake kwa uchumi wa dunia umefikia asilimia 36, akisisitiza kwamba kuna mambo matano inayozingatia katika kufikia maendeleo hayo, yakiwemo kuchukulia maendeleo ya kiuchumi kama kazi kuu na ya msingi, kuanzisha uchumi wa soko la kiujamaa kama mwelekeo wa mageuzi yake, kuhimiza kufungua milango kwa pande zote, kushikilia utawala wa sheria na kutafuta maendelo yanayotokana na uvumbuzi.