Rais Xi atuma salamu za pole kwa rais wa Nepal kufuatia ajali ya ndege
2023-01-18 10:23:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China Jumatatu alituma salamu za rambirambi kwa Rais Bidya Devi Bhandari wa Nepal kutokana na ajali ya ndege ya abiria iliyotokea nchini humo.

Katika salamu zake, Xi alisema baada ya kupata taarifa kuhusu ajali hiyo ambayo imesababisha hasara kubwa, angependa kutoa pole kwa familia zilizofiwa kwa niaba ya serikali na watu wa China.

Waziri Mkuu wa China Li Keqiang naye pia alituma salamu za rambirambi kwa mwenzake wa Nepal Pushpa Kamal Dahal.

Wakati mwili mwingine wa pili ukipatikana katika eneo la ajali katikati mwa nchi hiyo siku ya Jumanne, na kufanya jumla ya miili 71 kupatikana hadi sasa, mhanga wa mwisho bado hajathibitishwa kupatikana.

Ndege ya shirika la ndege la Yeti ilianguka kwenye korongo la Mto Seti karibu na mji wa Pokhara siku ya Jumapili ilipokuwa ikiruka kutoka Kathmandu kuelekea Pokhara ikiwa na watu 72.