China yasema inakaribisha ziara ya Blinken
2023-01-18 10:13:53| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema China inamkaribisha waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kufanya ziara nchini China, na pande mbili zinadumisha mawasiliano juu ya maandalizi husika.

Wang alisema hayo alipojibu kuhusu ripoti zinazosema kuwa Blinken atafanya ziara nchini China Februari 5 na kukutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang.

Wang alisema China siku zote inaangalia na kuendeleza uhusiano wake na Marekani kwa kufuata kanuni tatu za kuheshimiana, kuishi kwa amani, na kunufaishana. Amesisitiza kuwa China inaitaka Marekani kuwa na mtazamo sahihi kuhusu China, kushikilia mazungumzo kuliko mivutano, na kutafuta matokeo yatakayonufaisha pande zote mbili badala ya mchezo wa nipate usipate. China inatarajia kuwa Marekani itashirikiana na China katika kutekeleza kwa pande zote makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi mbili, na kurejesha uhusiano kati ya China na Marekani kwenye njia sahihi na nzuri na kuendelea kuwa tulivu.