UM wasema makaburi ya halaiki yapatikana mkoani Ituri, DRC
2023-01-19 09:31:50| CRI

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamegundua makaburi ya halaiki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambayo yana miili ya raia 42.

Kwa mujibu wa Farhan Haq, naibu msemaji wa Katibu Mkuu wa UM Antonio Guterres, wahanga hao wakiwa ni pamoja na wanawake 12 na watoto sita, walipatikana katika kijiji cha Nyamamba mkoa wa mashariki wa Ituri, na kwamba walinda amani pia wamegundua kaburi jingine likiwa na miili saba katika kijiji cha Mbogi.

Bw. Haq amesema Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) imepokea ripoti kwamba wanamgambo wa muungano huru wa wenye silaha (CODECO) walishambulia raia katika maeneo hayo wakati wa wikiendi na kuanzisha doria ili kufanya uchunguzi, na hapo ndio wakagundua makaburi hayo.