Awamu ya pili ya ujenzi wa JKCI kuanza Mloganzila
2023-01-19 13:45:10| cri

Serikali ya Tanzania na China zimesaini muhtasari wa upembuzi yakinifu wa ujenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Mloganzila, ikiwemo uboreshaji wa kituo bora cha magonjwa ya moyo Afrika Mashariki na Kati ambacho tayari kimejengwa.

Hafla hiyo ilifanyika jana jumatano, ambapo Tanzania iliwakilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu, na China iliwakilishwa na Mshauri wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, Chu Kun. Akizungumza baada ya hafla hiyo, Profesa Nagu ameishukuru Serikali ya China kwa hatua hiyo muhimu inayoleta matumaini katika kupanua na kurekebisha kituo hicho.

Kwa upande wake, Chu Kun amesema, hatua hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, kwani kwa kipindi kirefu madaktari wa Tanzania wamepelekwa China kwa ajili ya kuwaongezea uwezo, na madaktari wa China wanakwenda Tanzania kusaidia kutoa mtibabu kwa watanzania. Ameongeza kuwa, uboreshaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ulikuwepo katika mpango tangu mwaka 2018.