Rais wa Afrika Kusini atoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa serikali ya China na watu wake
2023-01-19 13:44:38| cri

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa salamu za sikukuu ya Mwaka Mpya wa jadi wa China kwa serikali na wananchi wote wa China.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Afrika Kusini imesema Rais Ramaphosa ametoa salamu hizo kupitia taarifa aliyotoa kwenye tovuti ya ikulu.

Kwenye taarifa hiyo Rais Ramaphosa amesema Afrika Kusini inathamini sana uhusiano mzuri wa kiuchumi na ushirikiano wa kisiasa ambao ni sifa ya ushirikiano kati yake na China.

Rais Ramaphosa pia amesema wakati China inakaribisha mwaka mpya wa Sungura, nchi hizi mbili pia zinaadhimisha miaka 25 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Watu wa China ulioanzishwa mwaka 1998.