Benki Kuu ya Sudan Kusini yazuia biashara kwa kutumia fedha za kigeni
2023-01-19 13:43:25| cri

Benki Kuu ya Sudan Kusini imezitaka taasisi za umma na sekta binafsi kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya nchi hiyo, Pauni ya Sudan Kusini (SSP), wakati bei ya ubadilishaji wa fedha ikiwa mbaya, ambapo sarafu ya nchi hiyo imeendelea kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani.

Gavana wa Benki Kuu ya Sudan Kusini Johnny Damian Ohisa ameuelekeza umma kufanya malipo yote kwa kutumia sarafu ya nchi hiyo, na kuongeza kuwa ni marufuku kwa taasisi yoyote, binafsi ama ya umma ndani ya nchi hiyo kufanya biashara kwa kutumia sarafu ya kigeni.

Gavana huyo amesema, bajeti ya umma, rekodi za fedha, na akaunti vinavyohitajika kisheria ama kuanzishwa na kuendeshwa nchini Sudan Kusini, vitafanyiwa tathmini kwa kutumia pauni ya nchi hiyo.