Rais Xi awasiliana na wananchi wa kada mbalimbali kwa njia ya video
2023-01-19 15:12:37| cri

Wakati sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China inakaribia, Rais Xi Jinping amezungumza kwa njia ya video na wananchi wa kada mbalimbali, wakiwemo matabibu walioko mstari wa kwanza wa kupambana na janga la COVID-19, wazee wanaoishi katika Nyumba za kutunza Wazee, wafanyakazi wa mashirika ya huduma za nishati, wafanyakazi na abiria katika vituo vya treni ya mwendo kasi, wafanyabiashara na wateja walioko katika soko la jumla la bidhaa za kilimo, na wakazi wa vijijini, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais Xi kuwasiliana na wananchi kwa njia hiyo.

Rais Xi amefuatilia sana kazi ya kudhibiti maambukizi na kutibu wagonjwa wa COVID-19, muda mfupi baada ya China kurekebisha sera zake za udhibiti wa janga hilo. Alipoongea na madaktari na wauguzi walioko mstari wa mbele, Rais Xi amepongeza mchango mkubwa walioutoa katika kulinda afya ya umma, na pia amewataka waimarishe hatua za kujikinga na kujitunza ili kulinda afya yao wenyewe.