Vikosi vya usalama vya Kenya vyawaua wapiganaji 10 wa al-Shabab katika mkoa wa mpakani
2023-01-19 09:28:34| CRI

Vikosi vya usalama vya Kenya Jumatano viliwaua wapiganaji 10 wa al-Shabab katika kaunti ya Garissa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Kamanda wa Polisi wa eneo la Kaskazini Mashariki George Seda alisema vikosi vya usalama kutoka mashirika mbalimbali vilifanya operesheni iliyoongozwa na idara ya ujasusi kwenye maficho ya al-Shabab huko Degbon baada ya kuwafuatilia watu hawa wenye itikadi kali kwa wiki moja.

Vikosi hivyo pia vilipata silaha zikiwa ni pamoja na maguruneti ya roketi (RPG), bunduki za AK-47, na vifaa vya vilipuzi.