UA walaani utekaji nyara wa zaidi ya wanawake 50 nchini Burkina Faso
2023-01-20 09:15:58| CRI

Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amelaani vikali kutekwa nyara kwa zaidi ya wanawake na wasichana 50 na watu wasiojulikana wenye silaha tarehe 12 na 13 huko Arbinda, mkoa wa Sahel, kaskazini mwa Burkina Faso .

Bw. Faki alitoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa watu hao waliotekwa nyara, na kurudi kwao salama kwa familia na jamii zao. Aidha amezitaka mamlaka nchini Burkina Faso kufanya juhudi zote na kuwafikisha mahakamani wahusika wa uhalifu huo wa kutisha.