China yatoa mpango kuhusu maendeleo ya kijani
2023-01-20 08:53:54| CRI

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka wa mpango wenye kichwa cha "Maendeleo ya Kijani ya China katika Enzi Mpya."

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutolewa kwa waraka huo jana alhamisi hapa Beijing, naibu mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Zhao Chenxin alisema waraka huo umeeleza hatua na mafanikio ya China katika maendeleo ya kijani katika muongo mmoja uliopita, na kufafanua mawazo na uzoefu wa nchi kuhusu maendeleo ya kijani. Waraka huo umesema kijani ni sifa kuu ya China katika enzi mpya, na maendeleo ya kijani yanatumika wakati China inajiendeleza kisasa.

Takwimu zimeonesha kuwa kuanzia 2012 hadi 2021, China ilipanda hekta milioni 64 za miti, kuzuia na kudhibiti hali ya jangwa zaidi ya hekta milioni 18.53 za ardhi, na kuongeza au kurejesha zaidi ya hekta laki 8 za ardhioevu. Nishati mbadala imekuwa na nafasi muhimu zaidi katika mchanganyiko wa nishati nchini China.