Makaburi ya watu wengi yagunduliwa mashariki mwa mkoa wa Ituri nchini DRC
2023-01-20 16:55:51| cri

Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema, askari wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa (MONUSCO) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamegundua kaburi walimozikwa raia 42.

Amesema katika kaburi la kwanza, maiti zilizokutwa ni za wanawake 12 na watoto sita, ziligunduliwa katika kijiji cha Nyamamba mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC, na kuongeza kuwa, askari wa kulinda amani pia waligundua kaburi lingine ilipozikwa miili ya wanaume saba katika kijiji cha Mbogi.

Bw. Haq amesema, MONUSCO ilipokea ripoti za mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la CODECO dhidi ya raia wikiendi, na kusema mashambulizi ya hivi karibuni yameongeza idadi ya watu wanaokimbia makazi yao na kufikia zaidi ya milioni 1.5 mkoani Ituri, na kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji.