Xi akagua utayari wa kupambana kwa vikosi vya jeshi
2023-01-20 08:53:03| CRI

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, Jumatano kupitia njia ya video, alikagua utayari wa kupambana kwa vikosi vya jeshi, kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

Rais Xi ametoa salamu za mwaka mpya kwa wafanyakazi wa huduma wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China na Jeshi la Polisi la Watu wa China, wafanyakazi wa kiraia jeshini, na jeshi la mgambo na la akiba.

Baada ya kuzungumza na vikosi mbalimbali juu ya utayari wao wa katika kazi mbalimbali zikiwemo kupambana, doria zao mipakani na kazi za usimamizi, rais Xi amewataka kuendelea kuwa macho na kuwa tayari kwa mapambano, kuchukua tahadhari na kudumisha usalama hasa katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China.

Aidha rais Xi amesema anatambua kikamilifu utayari wa mapambano wa vikosi mbalimbali, na kulitaka jeshi kutimiza majukumu yao kwa kulinda usalama wa taifa na utulivu wa jamii, ili kuhakikisha Wachina wanakuwa na sikukuu ya mwaka mpya ya furaha na salama.